map | search | help | download | contact us | français | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Tatizo Lililopo Jambo lenye athari kubwa zaidi kwa ziwa ni lile tishio kwa utajiri wake wa kibiolojia linalosababishwa na shughuli za mojawapo ya spishi mashuhuri - yaani binadamu. Ongezeko la kiwango cha mabadiliko ya mazingira yanayosababishwa na shughuli za binadamu sasa ni la kasi zaidi kupita uwezo wa fauna wa kujirekebisha kulingana na hali halisi. Ingawa kwa kweli watu wenyewe ni sehemu muhimu ya bioanuwai ya eneo hili, kuna hatari kubwa kwamba kutokana na athari zake bioanuwai itabadilishwa na kuwa biokiritimbi. Matatizo ya ziwa huanzia kwenye ardhi inayolizunguka. Miliki na wajibu wa kutunza ardhi ni wa mashaka na taarifa juu ya mbinu bora zaidi za utunzaji ardhi hazijawafikia wananchi, ambao wengi wao hawajapatiwa mafunzo yoyote ya kuwawezesha kutumia rasilimali zao kwa namna ambayo zinaweza daima zikajiendeleza. Watu hawa huyaona matatizo yao kama ni ya mara moja tu. Ufumbuzi wa matatizo haya, wa muda mfupi na mrefu, wa kibiolojia na kisosiolojia, wa kisheria na kiutendaji, lazima upatikane. Maarifa na ufahamu wa mambo changamani yanayoambatana na mabadiliko ya ekolojia vinahitajika ili kumuelimisha mnyama pekee mwenye uwezo wa kubadili kwa makusudi tabia zake na kuzifanya ziendane vilivyo na mazingira. Matatizo haya ndiyo yanayoshughulikiwa na mradi huu.
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|| Home || |
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Authors | Feedback |